Harakati za kutafuta amani Mashariki mwa Kongo zaendelea
25 Oktoba 2012Matangazo
Wakuu wa majeshi ya nchi hiyo wanakutana Goma, kupokea ripoti iliyochapishwa na jopo la maofisa wa ujasusi wa nchi za kanda hiyo. Hata hivyo, kikao cha wakuu wa majeshi kinaongozwa na mkuu wa jeshi la Uganda, Jenerali Alonda Nakairima, licha ya ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa, kuwa Uganda nayo inawafadhili waasi wa M23 mashariki mwa Kongo. John Kanyunyu na taarifa kamili kutoka Goma:
(Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: John Kanyunyu
Mhariri: Mohammed Khelef