Hali nchini mashariki mwa Kongo | Matukio ya Afrika | DW | 09.05.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Hali nchini mashariki mwa Kongo

Huku waasi wakiwa wametangaza kuundwa kwa chama chao kipya, waasi hao walionekana katika kijiji cha Kibiriga, kilomita zaidi ya ishirini kaskazini mwa mji wa Goma wakichimba mahandaki.

Bado hali si shwari mashariki mwa Kongo

Bado hali si shwari mashariki mwa Kongo

Mlio wa risasi pamoja na uwepo wa waasi katika kijiji hicho kwenye mpaka baina ya DRC na Rwanda, kulisababisha maelfu ya raia kuyahama makazi yao na kukimbilia Goma. Na wakati huohuo, generali muasi Bosco Taganda ametajwa kuwa amekimbilia katika mbuga ya Virunga, na kuacha vifaa vyake vya kijeshi vya zaidi ya tani ishirini.

John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Goma.

(Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)

Mwandishi: John Kanyunyu

Mhariri: Saumu Mwasimba

Sauti na Vidio Kuhusu Mada