Hakuna atakayemwaga chozi wakati Bush akiondoka madarakani. | NRS-Import | DW | 07.06.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Hakuna atakayemwaga chozi wakati Bush akiondoka madarakani.

Rais wa Marekani George W. Bush akizungumza katika bunge la Israel , Knesset May 18 , 2008.

Rais wa Marekani George W. Bush akizungumza katika bunge la Israel , Knesset May 18 , 2008.


Ni sawa kusema kuwa hakuna watu wengi watakaosikitika wakati rais George W. Bush atakapozuru Slovenia kuhudhuria mkutano wake wa mwisho katika kipindi chake cha urais baina ya umoja wa Ulaya na Marekani siku ya Jumanne Juni 10.Wakati wa utawala wake wa vipindi viwili katika ikulu ya Marekani, mahusiano baina ya Marekani na Ulaya yameonekana kuwa ya muhimu sana kwa Ulaya ambapo Donald Rumsfeld, waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani, alilielezea bara hili kwa msemo ambao ulikuja kuwa maarufu kuwa limegawanyika baina ya eneo kongwe na jipya. Lile kongwe kwa mujibu wa Rumsfeld, linapinga vita dhidi ya Iraq na lile jipya linaunga mkono.

Pamoja na hayo kunaonekana kuwapo na nia kutoka kila upande kwamba ushiriki wa Bush kwa mara ya mwisho akiwa nchini Slovenia usiharibiwa na hali ya kutokuwa na umoja.

Masuala muhimu yatajadiliwa, ikiwa ni pamoja na marufuku ya miaka 11 sasa dhidi ya mauzo ya nyama ya kuku katika umoja wa Ulaya, na ukweli kwamba Marekani inaruhusu raia wa baadhi ya mataifa ya umoja wa Ulaya lakini sio mengine kuingia katika ardhi yake bila visa. Mada nyingine nyingi nyeti , hususan zile zinazohusiana na haki za binadamu na kisiasa, zinaonekana kuepukwa, hata hivyo.

Dimitrios Papadimoulis , mjumbe wa mrengo wa shoto kutoka Ugiriki katika bunge la umoja wa Ulaya , ameutaka umoja huo kuibinya Marekani kufunga jela ya Guantanamo Bay, na kudai kuachwa mara moja kwa mpango wa utumiaji mateso, kuwekwa kizuizini na kutekwa nyara unaoendeshwa na shirika la ujasusi la Marekani CIA, kukiwa na madai kuwa linapata ushirikiano kutoka kwa baadhi ya serikali za umoja wa Ulaya.

Bunge la Ulaya linataka Guantanamo Bay ifungwe, amesema katika mjadala na wawakilishi wa serikali za umoja wa Ulaya pamoja na halmashauri ya Ulaya. Pia tunataka jela za siri zifungwe. Mtasema lolote kuhusu hilo kwa Wamarekani?

Sio halmashauri ya Ulaya ama serikali ya Slovenia , ambayo hivi sasa inashikilia kiti cha urais wa umoja huo , iliyojibu swali lake.

Emilou MacLean, mwanasheria katika kituo cha haki za kikatiba mjini New Yorj, ameshauri kuwa kuondoka kwa Bush madarakani hakutoi nafasi yoyote kwa mataifa ya Ulaya kuondoa umuhimu wa kufungwa kwa jela ya Guantanamo Bay.

Halikadhalika mabadiliko ya hali ya hewa ni suala ambalo linachafua sana uhusiano baina ya Marekani na umoja wa Ulaya, nalo hili litakuwamo katika ajenda za mkutano mjini Ljubiljana.

Kuhusu masuala la mabadiliko ya hali ya hewa, George W. Bush hataki kuweka nguvu za taifa hilo kubwa katika kupambana na tatizo hili. Marekani inaangalia zaidi uchumi wa taifa lake na kile inachoona hali bora ya wananchi wake kuliko kujali hali bora ya dunia.

Najua kuwa binadamu na samaki wanaweza kuishi pamoja kwa amani


licha ya kuwa Marekani ni taifa pekee lenye utajiri mkubwa wa viwanda kupuuzia mkataba wa Kyoto wa kupunguza utoaji wa gesi za carbon, upande wa Ulaya unamatumaini kuishawishi kuchukua jukumu muhimu zaidi katika juhudi za kupata mkataba utakaochukua nafasi ya ule wa Kyoto mara utakapomalizika.

Umoja wa Ulaya unatahadharishwa hata hivyo kutoweka nguvu zake kubwa katika kujadiliana na utawala ambao unaondoka madarakani, amesema na kuongeza kuwa mjadala halisi utafanyika wakati rais mpya ataingia ikulu ya Marekani.

►◄
 • Tarehe 07.06.2008
 • Mwandishi Kitojo, Sekione
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EFDv
 • Tarehe 07.06.2008
 • Mwandishi Kitojo, Sekione
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/EFDv
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com