Guendogan kuihama Borussia Dortmund | Michezo | DW | 02.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Guendogan kuihama Borussia Dortmund

Borussia Dortmund wanatarajiwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wake nyota kufuatia habari kuwa kiungo Ilkay Guendogan hataurefusha mkataba wake utakaokamilika mwaka ujao.

Klabu hiyo ya Bundesliga imewapoteza kiungo wa Ujerumani Mario Goetze na mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski waliojiunga na Bayern Munich katika mwaka wa 2013 na 2014.

Na baada ya kuwapoteza washambuliaji hao wawili, kiungo mweka mikakati Guendogan huenda akawa safarini mwishoni mwa msimu huu, japokuwa anakokwenda hakujulikani kwa sasa.

Dortmund inasema haijapokea maombi yoyote ya kutaka huduma za Guendogan, lakini vilabu kama Bayern, Manchester United, Arsenal na Juventus vyote vinamwinda nyota huyo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA/Reuters
Mhariri: Mohamed Daman