1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guardiola ataka kuendelea kuinoa Man City

21 Septemba 2020

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anasema anataka kuendelea kuitumikia klabu hiyo inayomilikiwa na mabwenyewe wa Uarabuni. City italenga kujaribu kuwapokonya Liverpool ubingwa wa ligi msimu huu

https://p.dw.com/p/3inmm
Pep Guardiola- Traîner Manchester City
Picha: picture-alliance/empics/PA Wire/M. Rickett

Pep Guardiola anasema anataka kuurefusha mkataba wake na Manchester City lakini lazima kwanza awadhihirishie wamiliki wa klabu hiyo ya Premier League kuwa anastahili mkataba mpya.

City inafungua kampeni yake ya msimu mpya leo dhidi ya Wolverhampton Wanderers na Guardiola mwenye umri wa miaka 49 amesema mabosi wa klabu hawajamuwekea shinikizo lolote tangu alipochukua usukani lakini anafahamu viwango vya klabu hiyo anapaswa kushinda mataji ili aurefushe mkataba. Pep ameshinda mataji mawili ya ligi tangu alipohamia Etihad 2016 na akasaini mkataba wa hadi 2021.

Wakati huo huo, Kiungo mshambuliaji wa Manchester City Ilkay Gundogan amekutwa na maambukizi ya virusi vya Corona akiwa mazoezini na wenzake kujiandaa na mchezo wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu nchini England dhidi ya Wolverhampton Wanderers Jumatatu 21.09.2020. Kiungo huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 29, atatakiwa kujitenga mwenyewe kwa siku 10 kabla ya kurejea tena na kandanda ya EPL.