Guardiola ashangazwa na timu yake
5 Machi 2018Sasa inahitaji ushindi mara nne tu katika michezo 9 ya mwisho kujihakikishia ubingwa. Kuweka umbali wa pointi 25 dhidi ya Chelsea, 33 dhidi ya Arsenal. Tottenham, Liverpool na Manchester United , zilipata matokeo mazuri na kuweka kasi nzuri. Hadi sasa tuko vizuri, nafikiri ni kutokana na vile tunavyocheza. Vile tunavyocheza hivi sasa kidogo ni sawa na kile tulichofanya msimu huu," alisema Pep Guardiola.
Ikiwa imebakia michezo 9 kumaliza msimu , City ambayo ina pointi 78 , ina nafasi ya kuwa timu ya kwanza kufikisha pointi 100 katika historia ya ligi ya England.
Nae kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema Marcus Rashford anapata uzoefu anaohitaji kusonga mbele na ukweli kwamba hajaanza mchezo katika kikosi cha kwanza tangu Desemba haitaathiri nafasi yake kuteuliwa katika kikosi cha taifa katika kombe la dunia. Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kwamba hali hiyo inasababisha kocha Southgate kupata wasi wasi wakati akijitayarisha kutaja kikosi chake kwa ajili ya michezo ya kirafiki dhidi ya Uholanzi na Italia.
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thiery Henry amesema hata kataa changamoto, iwapo nafasi itajitokeza kumrithi Arsene Wenger kuwa kocha wa washika bunduki Arsenal.
Hata hivyo , Henry ana shauku kwa raia mwenzake wa Ufaransa ambaye yuko katika kikaango , kuwa na "usemi wa mwisho" kuhusu kazi hiyo katika Arsenal ambayo ilianza wakati Wenger alipoanza kazi ya kuifunza klabu hiyo ya magharibi mwa London mwaka 1996.
Minong'ono ya muda mrefu kuhusu nafasi ya Wenger katika Arsenal iliongezeka baada ya kipigo cha nne mfululizo katika michezo yote na kipigo cha mabao 2-1 ugenini dhidi ya Brighton jana imezidi kusogeza karibu majaali yake ya kuondoka katika klabu hiyo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf , Saumu