Guardiola: Anfield bila mashabiki ni mahali tofauti | Michezo | DW | 08.02.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Guardiola: Anfield bila mashabiki ni mahali tofauti

Huko England Jumapili Liverpool walionyeshwa cha mtema kuni na Manchester City walipozabwa mabao 4-1 walipokuwa wakichuana na Manchester City.

Raia wa Ujerumani IIkay Gundogan kwa mara nyengine tena alifunga mabao mawili na kuendeleza mchezo wake mzuri msimu huu kwani ndiye mfungaji bora wa Manchester City kufikia sasa.

Kocha Pep Guardiola wa City lakini anasema amefurahishwa na ushindi ila kukosekana kwa mashabiki ndilo jambo la pekee alilojutia.

Fußball | Premier League | Manchester City - Crystal Palace

Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea goli lao

"La muhimu ni pointi tatu, bila shaka ninafurahishwa na wachezaji wangu kwasababu wamevunja rekodi baada ya muda mrefu. Natumai siku nyengine tutacheza vyema mashabiki wakiwa uwanjani kwasababu uwanja wa Anfield ni vitui viwili tofauti ukiwa na mashabiki na usipokuwa nao, kwasababu baada ya wao kusawazisha na mabao kuwa 1-1, unaweza kufikiria ingekuwaje," alisema Guardiola.

Mlinda lango wa Liverpool Alisson ambaye mara nyingi amekuwa akiwaokoa hao the Reds alifanya makosa makubwa jana na kusababisha timu yake kupoteza mechi hiyo na hapa kocha wa Liverpool Jurgen Klopp anazungumza kumhusu kipa huyo.

"Tatizo la makosa ni kwamba hujui utayafanya wakati gani, cha muhimu ni kujifunza kutokana na makosa na jambo hilo halitamtokea tena. Ametuokoa mara nyingi sana ila leo mambo yamekwenda vibaya kwa hiyo ni lazima tukiri tu," alisema Klopp.