Grace Kabogo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 10.02.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu ya DW

Grace Kabogo

Mfahamu Grace Kabogo, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

 1. Nchi ninayotokea: Tanzania
   
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: Julai 2009 - Juni 2011, kisha nikarudi tena Oktoba 2012
   
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilikuja kwa mafunzo ya miezi sita kuanzia Agosti 2008 hadi Januari 2009 kisha nikapata ajira.
   
 4. Kwa nini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Kwanza nilikuwa naipenda sana kazi ya utangazaji tangu nikiwa mtoto na nilivutiwa sana na utangazaji wa Deborah Mwenda, aliyekuwa akisimulia hadithi mbalimbali za Mama na Mwana. Pia nilitaka kuielimisha jamii kupitia masuala mbalimbali kwa kutumia taaluma yangu, kwa sababu ni kazi ambayo ina dhamana katika jamii.
   
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Kwanza aipende kazi yake. Aliyepata mafunzo ya kutosha kutoka kwenye vyuo husika vinavyotambulika. Awe mdadisi na mwenye kupenda kujifunza kulingana na mazingira. Afuate miiko na maadili ya uandishi wa habari. Azingatie weledi wa taaluma yake. Pia awe mkweli na atambue nafasi yake katika jamii.
   
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Kukosa ushirikiano kutoka kwa watendaji mbalimbali, pindi napotaka kuwahoji. Kuminywa kwa uhuru wa kufanya kazi kutokana na kuingiliwa kwa uhuru wa habari.
   
 7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela alipofunguliwa kutoka gerezani na kisha kuzuru Tanzania. Pia kifo cha Baba wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
   
 8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Nilitamani sana kumuhoji Papa Yohane Paulo II, lakini ndiyo haiwezekani tena kwa sasa. Lakini bado nina hamu ya kumhoji Papa.
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com