Gomez arejea katika timu ya Ujerumani | Michezo | DW | 29.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Gomez arejea katika timu ya Ujerumani

Kocha wa Ujerumani Joachim Löw amekiteua kikosi kipya kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa zikakazochezwa wiki ijayo. Orodha hiyo ina sura moja au mbili ambazo zitajaza nafasi za wachezaji waliostaafu

Sura kadhaa za zamani, na nyingine mpya za washindi wa Kombe la Dunia nchini Brazil, zitajumuishwa katika orodha mpya ya timu ya Ujerumani ikayocheza mechi mbili wiki ijayo mjini Dusseldorf na Dortmund.

Kati ya wachezaji wattau wanaorejea kikosini, mshangao mkubwa bila shaka ni kuitwa tena Mario Gomez. Mshambuliaji wa Bayern na Stuttgart, ambaye sasa anachezea klabu ya ligi ya ITALIA Serie A, fiorentina, alicheza kwa mara ya mwisho katika timu ya Ujerumani mnamo Agosti 2013. Kustaafu kwa Miroslav Klose bila shaka kumesaidia nafasi ya Gomez pamoja na mchezo wake mzuri katika ligi ya Italia.

Fußball DFB-Pokal 1. Runde: Stuttgarter Kickers - Borussia Dortmund

Mshambuliaji wa Dortmund Marco Reus pia ameitwa kikosini baada ya kuwa nje kutokana na jeraha

Beki wa Stuttgart Antonio Rüdiger pia amerejea kikosini, baada ya kustaafu Per Mertesacker. Marco Reus pia ameteuliwa na Löw, baada ya kupata jeraha kabla ya Kombe la Dunia. Lakini kwa jumla kikosi hicho cha wachezaji 21 kina wachezaji 18 walioshinda Kombe la Dunia.

Bastian Schweinsteiger na Shkodran Mustafi hawajajumuishwa katika kikosi cha Löw kuhusiana na matatizo ya majeraha. Philipp Lahm, Miroslav Klose na Per Mertesacker waliozitundika njumu zao karibuni wanatarajiwa kuagwa rasmi kabla ya mchuano wa kwanza.

Jumatano ijayo (03.09.2014) Ujerumani itachuana na Argentina mjini Dusseldorf katika mchuano wa kirafiki wa kimataifa, ikiwa ni kamamarudio ya fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Siku nne baadaye, Ujerumani itaelekea Dortmun kupambana na Scotland katika mechi yao ya kwanza ya kufuzu katika dimba la Ubingwa wa Ulaya mwaka wa 2016.

Kikosi kamili

Walinda lango: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hannover)

Mabeki: Jerome Boateng (Bayern Munich), Erik Durm (Dortmund), Matthias Ginter (Dortmund), Kevin Grosskreutz (Dortmund), Benedikt Höwedes (Schalke), Mats Hummels (Dortmund), Antonio Rüdiger (Stuttgart)

Viungo/Washambuliaji: Julian Draxler (Schalke), Mario Gomez (Fiorentina), Mario Götze (Bayern Munich), Christoph Kramer (Mönchengladbach), Toni Kroos (Real Madrid), Sami Khedira (Real Madrid), Thomas Müller (Bayern Munich), Mesut Özil (Arsenal), Lukas Podolski (Arsenal), Marco Reus (Dortmund), Andre Schürrle (Chelsea)

Mwandishi: Bruce Amani/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu