Germany-Georgia | Habari za Ulimwengu | DW | 23.08.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Germany-Georgia

Kansela Angela Merkel ahimiza paitishwe mkutano wa majirani za Georgia kulinda utulivu katika eneo hilo

Berlin:


Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anapendelewa paitishwe mkutano wa kimkoa wa majirani wa Georgia.Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari la Ufaransa AFP likimnukuu msemaji wa idara ya habari ya serikali kuu ya Ujerumani mjini Berlin.Katika toleo la jumatatu ijayo, jarida la Der Spiegel linasema kansela Angela Merkel ametoa pendekezo hilo kwa rais Nicholas Sarkozy,ambae nchi yake ndio mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa ulaya.Urusi haijaingizwa katika orodha ya nchi zinazotazamiwa kualikwa mkutanoni-amesema hayo msemaji wa wa idara ya habari ya serikali kuu.Mkutano huo utazungumzia ujenzi mpya na juhudi za kuimarisha utulivu nchini Georgia na katika eneo la kusini mwa Caucasus.Kansela Angela Merkel amepangiwa kuzitembelea Sweeden ,Estonia na Lithuania jumatatu na jummanne ijayo,ziara itakayogubikwa na mzozo wa Georgia na siasa ya nje ya Urusi.Viongozi wa eneo hilo wameelezea mshikamano wao pamoja na rais Mikhail Saakashvili wa Georgia.Ujerumani inajaribu kuendesha juhudi za kusawazisha hali ya mambo katika eneo la Caucasus.

 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3c7
 • Tarehe 23.08.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/F3c7
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com