Gedi ataka mazungumzo-Somalia | Habari za Ulimwengu | DW | 30.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gedi ataka mazungumzo-Somalia

MAGADISHU:

Waziri mkuu wa Somali Mohamed Gedi, leo amependekeza mazungumzo na mahasimu wa serikali yake –wafuasi wa kiislamu wa Mahkama za kisheria.Alionya wakihujumu ,serikali itawaandama.

Taarifa kutoka Geneva, Uswisi, zinasema watoto wenye umri kuanzia miaka 12, wanasajiliwa kupigana katika vita baina ya serikali ya Somalia na mahasimu wao -wanamgambo wa kiislamu-shirika la wakimbizi la UM limearifu.

Kati ya watu 55.000 na 60.000 wametimuliwa maskaini mwao na mapigano ya hivi karibuni nchini Somalia.

Kambi za kijeshi katika mikoa ya Bader,Barrawa na Manomofa- watoto wakiandikishwa.Kiasi cha wakimbizi 164 walivuka mpaka wa kaskazini-mashariki wa Kenya jana kutoka Somalia.Wengi wao ni watoto na wanawake kutoka eneo la kismayo ili kuokoa maisha yao. Kuna wakimbizi 170.000 wa kisomali nchini Kenya pekee kufuatia miaka 15 ya mapigano.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com