Gebrselassie ashinda Melbourn | Michezo | DW | 01.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Gebrselassie ashinda Melbourn

Hoffenheim imebakia kileleni mwa Bundesliga na Gebreselassie atamba Melbourn marathon.

default

IBISEVIC (Hoffenheim)

Bingwa wa rekodi ya dinia wa mbio za marathon,muethiopia Haile Gebrselassie,atoroka na ushindi wa Great Australian Run mjini Melbourne.

Taifa Stars ya Tanzania yatamba mbele ya Sudan ikiweka matumaini ya kwenda Abidjan mwakani kwa kombe maalumu la Afrika. Hoffenheim imebakia kileleni mwa Bundesliga ikiongoza kwa pointi 3 baada ya kuilaza Bielefeld jumamosi mabao 3:0.

Tukianza na Ligi mashuhuri za ulaya-Bundesliga-Premier League,La Liga ya Spian na Seriea A ya Itali,chipukizi wa Hoffenheim waliopanda msimu huu tu daraja ya kwanza ,wanaendelea kutamba katika Bundesliga.Wiki kabla ya changamoto yao na mabingwa Bayern Munich, Hoffenheim waliikomea Armenia Bielefeld mabao 3:0 ili kusalia kileleni.Wenzao Bayer Leverkusen waliokuwa pamoja kileleni waliteleza jumamosi walipozabwa mabao 2:0. Mpambano wa mwishoni mwa wiki ijayo kati ya Bayern Munich na Hoffenheim, utaamua nani atatawazwa mabingwa wa nusu-msimu kabla timu hazikuenda katika likizo ya X-masi na mwaka mpya.

Hivi ndivyo kocha wa Hoffenheim Ralf Reingnick alivyoueleza mpamba

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com