Gbagbo kushawishiwa aondoke! | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Gbagbo kushawishiwa aondoke!

Ujumbe wa viongozi kutoka nchi tatu za jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi Ecowas unawasili Abdijan leo.

Aliekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki katika juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Ivory Coast.

Aliekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki katika juhudi za kusuluhisha mgogoro wa Ivory Coast.

Ujumbe wa viongozi wa nchi za jumuiya ya uchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS unatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Ivory Coast, Abidjan leo ili kujaribu kumshawishi rais Laurent Gbagbo aondoke madarakani. Ujumbe huo ni wa viongozi kutoka,Benin,Sierra Leone na Cape Verde Jumuiya ya Ecowas imetishia kutumia nguvu ili kumwondoa Gbagbo madarakani ikiwa rais huyo atakataa kuondoka kwa hiari yake.

Wakati huo huo taarifa kutoka Abidjan zinesema wafanyakazi wengi wa mji huo waliupuuza mwito wa kushikiri katika mgomo wa nchi nzima uliotolewa na kiongozi wa upinzani Alassane Outtara anaetambuliwa kuwa mshindi wa uchaguzi .Vyombo vya habari vimearifu kuwa kazi ziliendelea kama kawaida kwenye bandari muhimu za Abidjan na San Pedro zinazotumika kusafirishia zao muhimu la kakao.Maduka yalifunguliwa na watu walienda ofisini.

 • Tarehe 28.12.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zqXu
 • Tarehe 28.12.2010
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/zqXu