Gbagbo haendi kokote
6 Aprili 2011Matangazo
Katika mahojiano yake ya simu na kituo kimoja cha televisheni cha Ufaransa, Laurent Gbagbo amekataa kumtambua Ouattara,mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Novemba mwaka jana nchini humo.
Gbagbo ametazamiwa kuondoka madarakani, baada ya viongozi wake wa kijeshi, kusalim amri hiyo jana, baada ya kushambuliwa vikali na wafuasi wa Ouattara waliosaidiwa na vikosi vya Ufaransa na Umoja wa Mataifa mjini Abidjan.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, Laurent Gbagbo amejificha katika kasri la rais mjini Abidjan.