Gaza:Mahmoud Abbas atawatuhubia wapalastina hii leo | Habari za Ulimwengu | DW | 16.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza:Mahmoud Abbas atawatuhubia wapalastina hii leo

Chama tawala katika maeneo ya wapalastina Hamas kinamtuhumu mshirika mkubwa wa rais Mahmoud Abbas,mkuu wa zamani wa vikosi vya usalama Mohammad Dahlan kuandaa njama ya kutaka kumuuwa waziri mkuu Ismail Haniya.Tuhuma hizo zimezidisha makali ya mvutano kati ya makundi hayo mawili hasimu ya wapalastina.Hamas wameamua kususia hotuba muhimu itakayotolewa hii leo na rais Mahmoud Abbas.Rais Mahmoud Abbas huenda ataitumia hotuba hiyo kuitisha uchaguzi wa kabla ya wakati katika maeneo ya utawala wa ndani wa Palastina.Wakati huo huo waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert akizungumza na kituo cha matangazo cha BBC amesema nchi yake iko tayari kuihama sehemu kubwa ya maeneo ya wapalastina ili kurahisisha utekelezaji wa mpango mpya wa amani ulioandaliwa na Marekani,Urusi,Umoja wa mataifa na Umoja wa ulaya.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com