Gaza-Sauti zinazidi kupazwa | Habari za Ulimwengu | DW | 04.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Gaza-Sauti zinazidi kupazwa

Walimwengu wanataka silaha ziwekwe chini haraka

Paris:Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anapanga kulitembelea eneo la mashariki ya kati licha ya kuzidi makali mzozo kati ya Israel na Hamas.Kuanzia kesho jumatatu raisRais Sarkozy anapanga kuzitembelea Israel,Misri,Utawala wa ndani,Syria,na Libnan,Rais Sarkozy anaanzia ziara yake mjini Jerusalem ambako atakua na mazungumzo pamoja na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert .Baadae atakwenda Charm el Sheikh kwa mazungumzo pamoja na rais Hosni Mubarak wa Misri,kabla ya kwenda Ramallah ambako amepangiwa kuzungumza na kiongozi wa utawala wa ndani Mahmoud Abbas.Wadadisi wanahisi ziara ya rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy inakabiliwa na kishindo kikubwa kutokana na kuzidi makali mzozo kati ya Israel na Hamas.Wakati huo huo Urusi sawa na jamhuri ya umma wa China zimeelezea wasi wasi wao kutokana na kuzidi makali mzozo huo.Viongozi wa mjini Moscow wamesema wanatuma ujumbe katika eneo la mashariki kwa lengo la kuhimiza silaha ziwekwe chini haraka.Mwito wa kuweka chini silaha haraka umetlewa pia na waziri mkuu wa Uengereza Gordon Brown.

 • Tarehe 04.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GRpS
 • Tarehe 04.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GRpS
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com