Gaddafi asema Walibya wako tayari kufa kumlinda | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.03.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Gaddafi asema Walibya wako tayari kufa kumlinda

Matamshi yake yamekosolewa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa akisema Gaddafi yuko mbali mno na ukweli halisi wa mambo nchini Libya

default

Gaddafi (kushoto)akisalimiana na Christiane Amanpour wa kituo cha habari cha ABC, mjini Tripoli

Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi amesisitiza kuwa raia wake wote wanampenda, hivyo kupuuza shinikizo la kimataifa linalozidi kumtaka aondoke madarakani na pengine akimbilie uhamishoni baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa miongo minne. Katika mahojiano yake hapo jana na televisheni ya ABC, BBC na gazeti la The Times la jijini London, Gaddafi amesema Walibya wako tayari kufa kwa ajili ya kumlinda na kusisitiza hakuna anayempinga. Gaddafi amedai hakuna maandamano yoyote mabarabarani.

Matamshi ya kiongozi huyo yamelaaniwa vikali na balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice.

Susan Rice

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice

Akizungumza katika ikulu ya Marekani mjini Washington, Bi Rice amesema matamashi hayo yanadhihirisha kwamba Gaddafi hafai kuongoza na amejitenga na ukweli halisi wa mambo. Wakati huo huo, Marekani imeanza jana kupeleka meli zake za kivita na ndege karibu na Libya. Marekani pia imezuilia mali za Libya za thamani ya dola bilioni 30 kumshinikiza Gaddafi aondoke madarakani.

Mwandishi: Josephat Charo

Mhariri: Aboubakar Liongo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com