Fury ambomoa Schwarz Las Vegas | Michezo | DW | 17.06.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Fury ambomoa Schwarz Las Vegas

Ushindi wa kishindo aliopata bondia Tyson Fur mjini Las Vegas mwishoni mwa wiki umemsogeza karibu na pigano la marudiano la kumezea mate na bingwa wa uzani wa juu Deontay Wilder

Ushindi wa kishindo aliopata bondia Tyson Fur mjini Las Vegas mwishoni mwa wiki umemsogeza karibu na pigano la marudiano la kumezea mate na bingwa wa uzani wa juu Deontay Wilder.

Muingereza Fury alimzidi nguvu na maarifa Mjerumani Tom Schwarz katika pigano la Jumamosi usiku, na ikambidi refarii asitishe kivumbi hicho kilichodumu dakika tano na sekunde 54. Fury akapata ushindi kwa njia ya knock-out. Kuna pigano moja zaidi linalopangwa kwa Fury Septemba au Oktoba, ambapo atataraji kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa na mpango kisha utakuwa ni kukutana tena na Mmarekani Deontay Wilder mapema 2020.

Wilder ndiye bingwa wa sasa wa taji la WBC, huku mataji ya WBA, WBO, na IBF yakishikiliwa na Andy Ruiz baada ya hivi karibuni kumduwaza Muingereza Anthony Joshua mjini New York.