Fujimori ameadhibiwa kufungwa jela miaka sita
12 Desemba 2007Matangazo
LIMA:
Rais wa zamani wa Peru,Alberto Fujimori ameadhibiwa kifungo cha miaka sita kwa hatia ya matumizi mabaya ya mamlaka.Mahakama katika mji mkuu Lima,imesema Fujimori alipokuwa madarakani, alitoa amri ya kusaka nyumba ya wakili mmoja bila ya kibali.
Fujimori mwenye umri wa miaka 69 anakabiliwa pia na mashtaka ya mauaji,ukiukaji wa haki za binadamu na rushwa.Yeye alitawala nchini Peru kuanzia mwaka 1990 hadi 2000 na alikimbilia Japan serikali yake ilipoanguka.