FREETOWN : Kura zaanza kuhesabiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 13.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FREETOWN : Kura zaanza kuhesabiwa

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini kote Sierra Leone baada ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi kupiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge hapo Jumamosi.

Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza tokea vikiosi vya Umoja wa Mataifa kuondoka nchini humo unaonekana kuwa ni mtihani wa kwanza kuona iwapo Sierra Leone imeibuka kikamilifu kutoka vita vyake vya wenyewe kwa wenyewe vya muongo mmoja. Waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Ulaya wamesema wameridhika na mchakato wa uchaguzi huo.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha APC Ernest Koroma anatazamiwa kumpa changamoto kubwa Makamo wa Rais Solomon Berewa wa chama tawala cha SLLP kwenye wadhifa wa urais.

Matokeo rasmi ya kwanza yanatazamiwa kutangazwa leo hii na iwapo hakuna mgombea wa urais atakayepata zaidi ya asilimia 55 ya kura uchaguzi huo utarudiwa mwezi wa Septemba.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com