Frankfurt yaibwaga Stuttgart na kusonga nafasi ya nne | Michezo | DW | 01.04.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Frankfurt yaibwaga Stuttgart na kusonga nafasi ya nne

Eintracht Frankfurt huenda ikacheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Luka Jovic alifunga tena na kupeana pasi ya bao jingine wakati Frankfurt ikiilaza Stuttgart 3 -0 na kusonga katika nafasi ya nne

Frankurt ilitumia kichapo cha Borussia Moenchengladbach cha 3 -1 dhidi ya Fortuna Düsseldorf Jumamosi, na kuchukua nafasi ya mwisho ya kufuzu Champions League zikiwa zimesalia mechi saba msimu kukamilika.

Katika mechi nyingine ya jana, bao la kipindi cha kwanza la Suat Serdar lilitosha kupunguza wasiwasi wa Schalke kushushwa ngazi, baada ya kuilaza Hanover 1 – 0.

Ulikuwa ushindi wa kwanza wa Schalke tangu kocha Huub Stevens aliporejea kwa mara ya tatu na unaiweka pointi sita juu ya eneo la kushushwa ngazi.Siku ya Jumamosi, Paco Alcacer alifunga mabao mawili katika dakika ya majeruhi na kuirejesha Borussia Dortmund kileleni mwa ligi kwa ushindi wa 2 – 0 dhidi ya Wolsfburg wakati Bayern Munich wakilazimika kutoka sare ya 1-1 na Freburg.