Ferrari yaapa kuwania ubingwa wa dunia | Michezo | DW | 18.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ferrari yaapa kuwania ubingwa wa dunia

Kiongozi mpya wa kikosi cha Ferrari Marco Mattiacci amesema timu yake haijakata tamaa katika kutwaa ubingwa wa dunia mwaka huu, ikiwa ni siku moja kabla ya mashindano ya mkondo wa Chinese Grand Prix.

Mattiacci alikuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza hapo jana baada a kuwasili China kwa mkondo wa Shanghai alipochukua nafasi ya Stefano Domenicali, aliyejiuzulu siku ya Jumatatu.

Wiki mbili zilizopita, madereva wa Ferrari Fernando Alonso na Kimi Raikknen walimaliza katika nafasi za tisa na kumi katika mkondo wa Bahrain Grand Prix, baada ya kushindwa kupambana na kasi ya timu zilizoongoza.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu