Federer ashinda taji la Australian Open | Michezo | DW | 29.01.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Federer ashinda taji la Australian Open

Roger Federer alidhihirisha kuwa wakati mwingine umri kwa kweli sio kitu michezoni, baada ya kushinda taji lake la tatu la Grand Slam katika mwaka mmoja. Na amesema hajui ataendelea kucheza hadi lini...

Mswisi huyo mwenye umri wa miaka 36 anaendelea kushamiri katika mchezo wa tenis baada ya kutinga fainali ya 30 ya mashindano makuu ya Grand Slam na kubeba ubingwa wa taji lake la sita la Australian Open na lake la 20 la Grand Slam.

Mchezaji huyo anayeorodheshwa nambari mbili ulimwenguni kwa upande wa wanaume alishinda mataji ya Australian Open mara mbili mfululizo kwa kumlaza jana Marin Cilic kwa seti za 6-2, 6-7, 6-3, 3-6 na 6-1. Federer alibubujikwa na machozi wakati akipewa kombe la ushindi "Bado sijielewi kwa sasa, kwamba yote yamekwisha na nimeweza kushinda tena…kufikisha mataji 20, na langu la sita hapa. mwaka huu umekuwa wa kushangaza tu. Siwezi kuamini nimeweza kutetea taji langu baada ya miaka hii yote, nimeweza kufanya hivyo tena. Sasa ni ushindi maalum na labda itachukua muda mrefu kwa hilo kuingia kichwani, sina uhakika. Hivyo ndio nnahisi kwa sasa.

Federer sasa amejiunga na Novak Djokovic na Muastralia Roy Emerson katika kikundi cha wachezaji walioshinda mataji sita ya Australian Open. Hongera zake na kila la kheri katika mashindano yajayo

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu