1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pliskova bingwa Brisbane International

7 Januari 2019

Roger Federer na Belinda Bencic kutoka Uswisi waliwabwaga Wajerumani Alexander Zverev na Angelique Kerber katika fainali ya Hopman cup kwenye mchezo wa tennis, iliyochezwa Jumamosi.

https://p.dw.com/p/3B9Mv
Australien Hopman Cup | Roger Federer
Picha: imago/J. Hasenkopf

 

Fainali hiyo ilichezwa siku ya Jumamosi. Lakini hii ndiyo makala ya mwisho ya kikombe hicho cha Hopman Cup kwa kuwa inafutiliwa mbali kutoka kwenye kalenda ya mashindano ya mchezo wa tennis.

Kwengineko mchezaji nambari moja wa zamani Karolina Pliskova alitoka chini kwenye mechi yake ya fainali ya Bribane International aliyokuwa anacheza na Lesia Tsurenko na kushinda kwa seti tatu za 4-6 7-5 6-2 hapo jana. Pliskova alikuwa na haya ya kusema baada ya mechi hiyo.

"Nilijihisi mchovu sana leo lakini nilijikaza na nikapambana. Bila shaka haikuwa rahisi kwasababu alikuwa anacheza vizuri na alikuwa anaweka shinikizo lote kwangu. Nilikuwa sichezi vizuri ila nilijikaza hadi mwisho na nilipata nafasi zangu kadhaa na nikazitumia na matokeo nikayapata," alisema Pliskova.

Mchezaji huyo pia anasema kwamba kocha wake Rennae Stubbs alichangia pakubwa kwa ushindi huo.

"Kawaida ni mtu anayefikiria mazuri kwa hiyo alinipa moyo wa kuendelea. Aliniambia alihisi kwamba nina uwezo wa kuyageuza matokeo ya mechi hii na kwamba bado naweza kuebuka mshindi. Nilikuwa sihisi hivyo kwa hiyo ilinisaidia alipoyasema maneno hayo na labda ndiyo sababu nilishinda," alisema bingwa huyo.

Na kwa kauli hiyo ya Karolina Pliskova ndiyo nafika mwisho wa michezo kwa leo. Kwa mengi zaidi tembelea tovuti yetu dw.com, mimi ni Jacob Safari.

Mwandishi: Jacob Safari/APE/AFPE/DPAE

Mhariri: Gakuba Daniel