1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Aldin Mutembei
Dk. Aldin Mutembei wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Picha: Mohammed Khelef

Fasihi ya Kiswahili katika zama za TEKNOHAMA

Mohammed Khelef
9 Julai 2014

Wakati teknolojia ya habari na mawasiliano ikizidi kuimarika na kuchukua nafasi ya njia kongwe za mawasiliano, fasihi ya Kiswahili nayo inajikuta kwenye changamoto ya kuakisi mabadiliko ya wakati.

https://p.dw.com/p/1CYfM

Dk. Aldin Mutembei wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (TATAKI) anazungumzia nafasi ya fasihi ya Kiswahili kwenye zama hizi mpya za mawasiliano, ambapo mitandao ya kijamii imekuwa jukwaa kubwa kabisa la mawasiliano.

Kwa mujibu wa Dk. Mutembei, fasihi ya Kiswahili haijapitwa na kasi ya teknolojia mpya na badala yake imekuwa ikienda sambamba na mageuzi kwenye jukwaa hili la mawasiliano. Hata hivyo, mtaalamu huyo wa fasihi anakiri kwamba kuna changamoto kadhaa ambazo wanafasihi wa Kiswahili wanapaswa kukabiliana nazo ili uasili wa fasihi ya Kiswahili isipotee.

Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mhariri: Mohamed Abdulrahman

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi