1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fainali ya kombe la shirikisho Julai 4

Josephat Charo
11 Mei 2020

Fainali ya kombe la shirikisho la Ujerumani, DFB Pokal, ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika Mei 23 mjini Berlin, imeahirishwa hadi Julai 11 bila mashabiki kuwepo uwanjani.

https://p.dw.com/p/3c30c
Generalversammlung der DFL Fritz Keller
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gora

Shirikisho la soka Ujerumani DFB limesema Jumatatu (11.05.2020) kwamba mechi za nusu fainali za kuwania kombe hilo zitachezwa Juni 9 na 10. Mabingwa watetezi Bayern Munich watawakaribisha nyumbani Allianz Arena Eintracht Frankfurt huku Bayer Leverkusen wakiwa wenyeji wa Saarbruecken katika uwanja wa BayArena mjini Leverkusen.

Hata hivyo rais wa DFB, Fritz Keller, alisema mipango yao kubadilisha ratiba ya mashindano ya kombe hilo bado inasubiri kuidhinishwa na serikali ya kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.

Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga, inarejea viwanjani Mei 16 wakati itakapokuwa ligi ya kwanza kubwa ya Ulaya kurejea tena licha ya janga la vírusi vya corona ambalo limesababisha vifo vya watu takriban 7,500 Ujerumani.

"Mipango yetu inaendelea ili tuukamilisjhe msimu wa mashindano haya uwanjani kwa njia inayofaa," alisema Keller, huku mechi ya fainali ikitarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Olympic Stadium mjini Berlin.

(afp)