17 Agosti 2020
Matangazo
Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi kuhusu ugonjwa wa homa ya manajano, binadamu anapata maradhi hayo baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi. Mbu hao wako katika sehemu za joto, barani Afrika na Amerika ya Kusini. Ikiwa mtu anaambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ini lake pamoja na viungo vingine vya ndani vinaweza kudhurika na kusababisha kifo. Kwa mengi zaidi unganana na Zainab Aziz katika makala ya Afya Yako.