1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Elon Musk kushitakiwa Brazil

8 Aprili 2024

Jaji wa Mahakama ya Juu ya Brazil, Alexandre de Moraes, ameanzisha uchunguzi dhidi ya mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, Elon Musk.

https://p.dw.com/p/4eWWm
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, Elon Musk.
Mmiliki wa mtandao wa kijamii wa X, Elon Musk.Picha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Musk anatuhumiwa kwa kuzuwia sheria kuchukuwa mkondo wake.

Mmiliki huyo wa mtandao wa X anapingana na uamuzi wa Jaji Moraes ulioutaka mtandao huo wa kijamii kuzifungia baadhi ya akaunti za watumiaji.

Soma zaidi: Twitter yaondowa alama ya buluu kwenye akaunti za watu mashuhuri

Mapema hapo jana, Musk alituma ujumbe kwenye mtandao huo akisema X itaondowa zuio dhidi ya watumiaji hao kwa kuwa ni kinyume na katiba.