Elizabeth Shoo | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 20.04.2017
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu ya DW Kiswahili

Elizabeth Shoo

Mfahamu Elizabeth Shoo, mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW

 1. Nchi ninayotokea: Tanzania
 2. Mwaka nilipojiunga na DW: 2011
 3. Nilivyojiunga na DW: Nilipokuwa mwanafunzi wa chuo kikuu mjini Cologne, nilikuja kufanya mazoezi ya miezi mitatu DW. Baadaye nikaanza kufanya kazi mara kwa mara katika Idhaa ya Kiswahili na nilipomaliza chuo nikajiunga moja kwa moja na DW.
 4. Kwa nini niliamua kuwa mwandishi wa habari: Tangu nilipokuwa shuleni nilikuwa mtu anayependa kuandika, kusoma kuhusu matukio mbalimbali na pia kutangaza. Nilipomaliza sekondari nikaamua kusoma uandishi wa habari na kutimiza ndoto yangu.
 5. Vigezo mtu anavyotakiwa kuwa navyo kuwa mwandishi wa habari: Ili kufanya kazi ya uandishi wa habari vizuri mtu lazima awe mdadisi, mchapa kazi, mtu anayethubutu kuuliza maswali na aliye tayari kujifunza mambo mapya kila siku.
 6. Changamoto ninazokutana nazo kwenye maisha yangu ya kazi: Upatikanaji wa habari siku hizi umekuwa mrahisi mno. Mtu yeyote anaweza kuingia kwenye mitandao ya kijamii na kuandika habari. Changamoto kwa waandishi wa habari ni kutambua habari za kweli na kuzitofautisha na zile ambazo ni feki.
 7. Tukio la kihistoria ambalo sitalisahau: Kuchaguliwa kwa Donald Trump kuwa Rais wa Marekani. Lilikuwa tukio ambalo watu wachache sana walitarajia kuwa lingeweza kutokea.
 8. Mtu ambaye ningependa kumhoji: Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com