DUBAI:Mkenya ajificha kwenye kasha | Habari za Ulimwengu | DW | 06.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI:Mkenya ajificha kwenye kasha

Raia mmoja wa Kenya amejaribu kutoroka Emarati kwa kujificha kwenye kasha la mbao ili kusafirishwa kama mzigo nje ya nchi hiyo.Jaribio hilo halikufaulu baada ya ndege aliyokuwemo kucheleweshwa kwa saa kadhaa.

Mwanamume huyo ambaye jina lake bado halijulikani ni mfanyikazi wa zamani katika kampuni ya mizigo katijka uwanja wa ndege wa Dubai alipakia maji,chakula na hewa ya oxygen kwenye chupa ili aweze kutoroka hadi mjini Eldoret nchini Kenya.

Baada ya ndege hiyo kucheleweshwa kwa saa kadhaa mtu huyo aliyanza kugonga kuta za kasha hilo ili kutolewa.Maafisa wa forodha waliarifiwa na kumkamata na kupelekwa polisi.

Kwa mujibu wa polisi hati ya kusafiria ya mtu huyo inazuiliwa na serikali ya Emarati kwani alivunja sheria kabla hapo.Mtu huyo alishajribu kutoroka nchini humo bila hati ya kusafiria.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com