1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC: Wabunge waeleza mashaka yao juu ya kuongezeka wanajeshi

Jean Noel Ba-Mweze23 Aprili 2021

Wabunge wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameelezea mashaka yao kuhusu kuongezeka wanajeshi wa kigeni kuongezeka katika eneo hilo.

https://p.dw.com/p/3sV2B
DRK Symbolbild FARDC
Picha: Alain Wandimoyi/AFP

Rais Félix Tshisekedi mnamo siku ya Jumatano alitangaza ujio wa wanajeshi wa Kenya ambao wanatarajiwa hivi karibuni kuingia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Kongo kupambana na ugaidi na kuzima vurugu katika eneo hilo la Mashariki.

Baadhi ya wabunge wa kitaifa walishangaa kumsikia Rais Félix Tshisekedi akieleza kwamba, wanajeshi wa Kenya wanatarajiwa hapa wiki chache zijazo.

Jambo kama hilo la kuwaingiza askari wa kigeni hapa nyumbani ni lazima lijadiliwe bungeni kulingana na katiba ya nchi, lakini hili halikufuata utaratibu wa kawaida, kama anavyoeleza Juvenal Munubo, mbunge toka eneo la Walikale mkoani Kivu ya Kaskazini.

Nairobi Angriff auf Hotel in Kenias Hauptstadt
Vikosi vya usalama vya KenyaPicha: picture-alliance/AP Photo/B. Curtis


"Kama wanaingia kupitia mapatano ya kiaskari kati ya Kongo na Kenya, sherti wabunge waruhusu kuingia kwa majeshi za kigeni. Kwani, tumepata habari kusema wanyarwanda wameingia, waganda wameingia, lakini hakujakuwa hata mazungumzo kuhusu swali hilo katika bunge letu. Na ndiyo maana, ni sherti president wa inchi afanye angalisho kuheshimu katiba ya inchi hii."

Kwa muda mrefu sasa vikosi vya kigeni vimekuwepo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lakini maeneo mengi bado yanaendelea kukumbwa na ukosefu wa usalama kwa miongo kadhaa.

Soma zaidi: Vijana DRC waandamana dhidi ya MONUSCO

Mauaji yanaripotiwa karibu kila leo huko Kivu ya Kaskazini na Ituri pia kwenye mikoa mingine. Mashambulizi hufanywa nawatu wanaotoka kwenye makundi yanavyomiliki silaha.

Kwa mujibu wa Profesa Nkere Ntanda wa Chuo Kikuu cha Kinshasa, mamlaka inapaswa kuacha kuwategemea wanajeshi wa kigeni na badala yake, kulishughulikia ipasavyo kulijenga jeshi la taifa.

"Majeshi za kigeni zimekuwa ndani ya Kongo miaka ishirini. Hata solution moja haijapatikana. Na ndiyo hivi, kwa kuleta amani ndani ya Kongo inabidi rais na Jamhuri wajikaze kujenga jeshi la Kongo ambalo litajitegemea na kupiganisha hawa waasi ambao hawamaliziki, haswa ndani ya Kivu."

Wakaazi wengi wa mashariki mwa Kongo wanaendelea kuitaka tume ya Umoja wa mataifa nchini Congo (Monusco) kuondoka nchini humu.