DRC: Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu Waasi wa M23 | Matukio ya Afrika | DW | 14.01.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

DRC: Ripoti ya umoja wa mataifa kuhusu Waasi wa M23

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeelezea wasiwasi wake kufuatia ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo inasema waasi wa M23 wanaendelea kuwasajili wapiganaji katika nchi jirani za Rwanda na Uganda.

Waasi wa M23

Waasi wa M23

Serikali ya Kongo imeomba kuwepo na uchunguzi wa kina na uendeshwe na Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu, ICGLR, na Umoja wa Mataifa kuhusu madai hayo. Wakati huohuo serikali ya DRC imetoa wito kwa Rwanda na Uganda kutekeleza mkataba wa amani wa Addis-Ababa baina ya nchi za Maziwa Makuu. Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo. Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Salehe Mwanamilongo

Mhariri: Mohamed Khelef

Sauti na Vidio Kuhusu Mada