DRC: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru | Matukio ya Afrika | DW | 30.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

DRC: Maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru

Upinzani Katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo umesema rais Joseph Kabila hajaonyesha nia ya wazi ya kuweko na uchaguzi mkuu nchini humo.

Joseph Kabila Kabange

Rais Joseph Kabila

Rais Kabila ambae amelihutubia taifa katika madhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Kongo leo , amesema kwamba uchaguzi ujao utakuwa wa utulivu na amani , huku akiwaomba wapinzani kushiriki kwenye mazungumzo ya kitaifa ili kujadili changa moto za uchaguzi.Hata hivyo Kabila ambaye hakutaja ikiwa atagombea au la, ametupilia mbali pendekezo la kuweko na msuluhishi wa kimataifa katika mazungumzo hayo kama wanavyodai wapinzani.
Taarifa kamili na mwandishi wetu Saleh Mwanamilongo.

Mwandishi Saleh Mwanamilongo

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Sauti na Vidio Kuhusu Mada