Dortmund yateleza kileleni, Bayern wapunguza mwanya | Michezo | DW | 11.02.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dortmund yateleza kileleni, Bayern wapunguza mwanya

Borussia Dortmund ilitupa uongozi wa 3 - 0 na kutoka sare ya 3- 3 na Hoffenheim, huku Bayern nao wakipata ushindi dhidi ya Hertha Berlin na kupunguza mwanya

Ilikuwa wikiendi ambayo kwa mara ya kwanya vinara wa ligi Borussia Dortmund walionyesha kuyumba. Walipoteza uongozi wa 3 -0 zikiwa zimebaki dakika 25 mechi kumalizika na kutoka sare ya 3 – 3 na Hoffenheim. Ni kitu cha kutia wasiwasi hasa katika safi yake ya ulinzi. 

Wakati Dortmund wakitoka sare, kuna timu ilikuwa ikiwaangalia tu. Bayern Munich, na walilifahamu kuwa ushindi kwao ungewapunguzia pengo hadi pointi tano tu na wakaifyekelea mbali Schalke 3 – 1.

Kitu kingine kilichojitokeza mwishoni mwa wiki ni kuwa Peter Bosz na Bayer Leverkusen inaonekana kuwa ndoa nzuri kabisa. Mfumo wa kushambulia zaidi anaoupendelea Bosz uliifagilia Mainz kwa kichapo cha 5 -1. Amini usiamini, Leverkusen imesonga hadi nafasi ya sita na wanachungulia sasa kandanda la Ulaya.

Wikiendi haikuwa nzuri hata hivyo kwa Borussia Moenchengladbach, ambapo walikuwa wametoshana na Bayern katika nafasi ya pili kabla ya kukaangwa na Hertha Berlin ambao waliwafunga 3 - 0.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Josephat Charo