Dortmund yamsajili Gonzalo Castro kutoka Leverkusen | Michezo | DW | 25.05.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dortmund yamsajili Gonzalo Castro kutoka Leverkusen

Klabu ya Borussia Dortmund imetangaza kuipata sahihi ya kiungo wa Ujerumani Gonzalo Castro kutoka klabu ya Bayer Leverkusen. Castro amesaini mkataba wa miaka minne

Inaripotiwa kuwa Castro amenyakuliwa kwa kiasi cha euro milioni 11 kutoka BayArena.

Mkiurugenzi wa michezo wa BVB Michael Zorc amesema kwenye tovuti ya klabu hiyo kuwa wamefurahia kumsajili kiungo mwenye ujuzi, kipaji cha kiufundi ambaye anaweza kutumiwa katika nafasi tofauti uwanjani.

Castro, mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Leverkusen akiwa na umri wa miaka 14 mnamo mwaka wa 2002 na akaichezea klabu hiyo mechi 370 baada ya kuibuka kutoka timu ya vijana. Pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara tano.

Castro ndiye mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Dortmund mwishoni mwa msimu huu na mchezaji wa kwanza kujiunga na klabu hiyo kabla ya Thomas Tuchel kuwasili kama kocha mpya msimu ujao.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu