1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Domenico Tedesco amwaga wino RB Leipzig

9 Desemba 2021

Domenico Tedesco ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa RB Leipzig siku nne baada ya kuondoka Mmarekani Jesse Marsch.

https://p.dw.com/p/4433d
Domenico Tedesco | wird neuer Trainer bei RB Leipzig
Picha: Elmar Kremser/SVEN SIMON/picture alliance

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo, Tadesco mwenye umri wa miaka 36, mkufunzi wa zamani wa Schalke 04 na Spartak Moscow ametia saini mkataba hadi mwaka 2023 na Jumamosi hii atakuwa kwenye benchi la ukufunzi akitazama mechi dhidi ya Borussia Moenchengladbach.

Tadesco alikuwa pia kocha wa zamani wa vijana wa Hoffenheim na VfB Stuttgart. Ni raia wa Ujerumani mzaliwa wa Italia, ana uzoefu mdogo wa Bundesliga, akiwa amekaa chini ya misimu miwili Schalke. Aliondoka Spartak mapema mwaka huu.

Tedesco, aliiongoza Schalke hadi nafasi ya pili kwenye Bundesliga mnamo 2018 na kufukuzwa kazi mnamo 2019, lakini pia alimaliza katika nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Urusi na timu ya Spartak mara ya mwisho, na aliondoka Moscow kutokana na sababu za kifamilia.

Kocha huyu hakuwahi kucheza soka kitaaluma kabla ya kuwa mkufunzi, alivutia wengi akiwa na timu ya daraja la pili ya Ujerumani Erzgebirge Aue katika mechi yake ya kwanza kabla ya kujiunga na Schalke.

Leipzig wameonyesha nia yao kutumia makocha wenye umri mdogo kwa kumchagua Julian Nagelsmann miaka miwili iliyopita na sasa wamechukua uamuzi kama huo.

 

//Reuters, Dpa