1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Djokovic mfalme wa tennis

22 Februari 2021

Novak Djokovic ameshinda taji lake la 18 la Grandslam baada ya kuebuka bingwa wa Australian Open hapo Jumapili. Alimbwaga Daniil Medvedev kwa seti tatu za 7-5 6-2 6-2.

https://p.dw.com/p/3phzF
Tennis | Australian Open | Daniil Medvedev - Novak Djokovic
Picha: William West/AFP/Getty Images

 Kwa sasa anasema anataka kupumzika tu ili apone jeraha alililopata.

"Nimetoka kufanyiwa uchunguzi mwengine wa MRI hivi asubuhi na kwa kweli nimeumia sana kuliko nilivyochunguzwa mara ya kwanza. Lakini kutokana na alichokisema daktari, sijaumia sana lakini nitachukua mapumziko ili nipone. Msuli umekatika pakubwa," alisema Djokovic.