Djokovic apewa taji baada ya Federer kujiondoa | Michezo | DW | 17.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Djokovic apewa taji baada ya Federer kujiondoa

Fainali iliyosubiriwa kwa hamu ya mwisho wa msimu ilikamilika hata kabla ya kuanza wakati Roger Federer alipolazimika kujiondoa kutokana na jeraha kabla ya fainali ya ATP World Tour na Novak Djokovic

Mswisi huyo mwenye umri wa miaka 33, ambaye alimbwaga mwenzake Stanislas Wawrinka katika nusu fainali usiku uliotangulia, alitangaza uamuzi huo katika uwanja wa O2 Arena uliokuwa umerufika kwa ajili ya fainali hiyo.

Hivyo basi Djokovic anayeorodheshwa nambari moja ulimwenguni katika mchezo wa tennis kwa wanaume, ndiye mchezaji wa kwanza wa Tennis kushinda Finali hizo za ATP World Tour kwa miaka mitatu mfululizo lakini hakuonekana kuwa mwenye furaha wakati akipokea kombe pamoja na hundi ya dola milioni 1.92… labda kwa sababu hakuutolea jashi ushindi huo…

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com