​​​​​​​Djokovic amwangusha Murray | Michezo | DW | 09.01.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

​​​​​​​Djokovic amwangusha Murray

Novak Djokovic aliuwekea kikomo ushindi wa mechi 28 mfululizo wa mchezaji anayeorodheshwa nambari moja duniani Andy Murray, mjini Doha hapo jana na kuhifadhi taji la mashindano ya Qatar Open

Nyota huyo Mserbia Djokovic alishinda 6-3, 5-7, na 6-4 katika mchuano huo wa ubora wa juu uliodumu masaa matatu kati ya wachezaji hao bora kabisa duniani

Ulikuwa ushindi wa 25 wa Djokovic dhidi ya Murray na unatuma ujumbe wa mapema msimu huu dhidi ya mpinzani huyo wake mkuu Muingereza, kabla ya mashindano ya Australian Open baadaye mwezi huu.

Murray hata hivyo amesema kichapo hicho hakitakuwa na athari yoyote kwa juhudi zake za kutwaa ubingwa wa Australian Open kwa mara yake ya kwanza. Mashindano hayo yataanza Januari 16.

Mwandishi: Bruce Amani/AFPDPA
Mhariri:Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com