Djokovic ampiku Jo-Wilfred Tsonga mjini Shanghai | Michezo | DW | 19.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Djokovic ampiku Jo-Wilfred Tsonga mjini Shanghai

Katika tennis, Mserbia Novac Djokovic alibwaga Jo-Wilfred Tsonga katika fainali za kinyang'anyiro cha taji la Shanghai.

Djokovic alidhihirisha kuwa bado yeye ni mchezaji nambari moja Duniani baada ya kutawala katika mchezo huo wa hapo jana na kumshinda Tsonga kwa seti 6,2 6,4.

Djokovic mpaka sasa ameshinda seti 22 na hajafungwa katika mechi 17 alizocheza na hiyo ni rekodi yake tangu kuanza kwa mashindano ya wazi ya Marekani. Mpaka sasa ameshinda mataji 25 ikiwa ni moja zaidi ya Roger Federer. Amepungukiwa na mataji mawili tu akimfikia anayeshikilia rekodi kwa sasa Rafael Nadal.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu