Diego Costa asema yeye sio malaika | Michezo | DW | 23.10.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Diego Costa asema yeye sio malaika

Anafahamika kama mtukutu na baadhi ya watu, lakini mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amesema kuwa hatobadili kamwe mtindo wake wa kimabavu wa kucheza ndiposa aweze kupata marafiki wapya

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Uhispania mzaliwa wa Brazil amepata sifa ya kuwa mchokozi uwanjani tangu alipowasili katika klabu ya Chelsea ambako magoli yake 20 yaliisaidia kutwaa taji la ligi ya Premier mwaka jana.

Msimu huu anaonekana kupungukiwa na magoli, na anasema lengo lake kuu ni kuisaidia timu yake na sio kujiwekea picha ya kuwa kijana mzuri.

Katika mahojiano na BBC, Costa amesema na hapa namnukuu, “watu wengine wanadhani kandanda ni kama mchezo wa kuigiza, na kwamba kila mtu lazima acheze jukumu la kijana mzuri”. Anasema alifika hapo alipo kwa sasa kutokana na namna anavyocheza, na hatobadilika kwa sababu ya maoni ya watu wengine.

Hata hivyo Costa amesema yote hayo anayafanya tu wakati akiwa uwanjani, lakini yeye ni kijana mtulivu sana na mcheshi wakati anapokuwa na jamaa na marafiki nyumbani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu