1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Didavi kubaki Stuttgart msimu ujao

Josephat Charo
18 Mei 2021

Kiungo mshambuliaji wa Stuttgart Daniel Didavi ataendelea kuichezea klabu hiyo ya Bundesliga hadi mwaka 2022.

https://p.dw.com/p/3tYtV
Bundesliga | VfB Stuttgart v FC Augsburg
Picha: THOMAS KIENZLE/AFP/Getty Images

Kiungo mshambujliaji Daniel Didavi ataendelea kuichezea klabu ya VfB Stuttgart kwa angalau msimu mmoja mwingine baada ya kurefusha mkataba wake hadi 2022. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa Jumanne. (18.05.2021)

"Mimi ni wa hapa na nina furaha sana kuhusu hilo," alisema Didavi, mwenye umri wa miaka 31 aliyepitia mfumo wa soka la vijana Stuttgart na kurejea kuichezea klabu hiyo baada ya kuichezea Wolfsburg kwa kipindi kifupi kati ya mwaka 2016-2018.

(dpa)