1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Asili na mazingiraUmoja wa Falme za Kiarabu

Dhahabu ya mabilioni ya dola husafirishwa kwenda UAE

30 Mei 2024

Usafirishaji haramu wa dhahabu nje ya Afrika hasa kuelekea katika Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE umeongezeka katika kipindi cha miaka kumi iliyopita

https://p.dw.com/p/4gR7h
Mchimbaji madini kutoka Tanzania Assia Hussein, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha wachimbaji madini wanawake, akiangalia baadhi ya madini ya dhahabu katika soko la dhahabu mjini Geita, Tanzania Mei 28, 2022.
Mchimbaji mgodi wa Tanzania Assia Hussein aangalia baadhi ya madini ya dhahabu katika soko la dhahabu mjini Geita, TanzaniaPicha: LUIS TATO/AFP

Usafirishaji haramu wa dhahabu kutoka Afrika umeelezwa katika ripoti iliyochapishwa leo na shirika la  Swissaid, linaloangazia misaada ya maendeleo na uhamasishaji.

Dhahabu ya thamani ya dola bilioni 30 ilisafirishwa mwaka 2022

Uchambuzi uliofanywa na Swissaid, umegundua kuwa jumla ya tani 435 za dhahabu, inayochimbwa zaidi na wachimbaji migodi wadogo na yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 30, ilisafirishwa nje ya Afrika mnamo mwaka 2022.

UAE ni kituo kikuu cha dhahabu kutoka Afrika

Swissaid imesema UAE ndio kituo kikuu cha dhahabu hiyo kutoka Afrika na kwamba muongo mmoja awali, ilipokea zaidi ya tani 2,500 za dhahabu yenye thamani ya jumla ya zaidi ya dola bilioni 115.