1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DFB yafuta uanachama wa heshima wa Gerhard Schroeder

11 Machi 2022

Chama cha kandanda nchini Ujerumani - DFB kimeungana na klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund Borussia Dortmund kwa kuufuta uwanachama wa heshima wa aliyekuwa kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder.

https://p.dw.com/p/48MhA
Schröder gratuliert Putin zum 53. Geburtstag
Picha: EPA/ITAR-TASS/dpa/picture alliance

Chama cha kandanda nchini Ujerumani - DFB kimeungana na klabu ya Bundesliga Borussia Dortmund Borussia Dortmund kwa kuufuta uwanachama wa heshima wa aliyekuwa kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder juu ya mahusiano yake na Urusi. Kaimu rais wa DFB Rainer Koch amesema shambulizi la Urusi dhidi ya Ukraine ni kinyume na sheria ya kimataifa na kwa hivyo haliendani na maadili ya DFB.

Na kwa bahati mbaya, Schroeder hajaitikia miito mingi iliyotolewa kwake ya kumtaka achukue msimamo wa wazi dhidi ya vita hivyo. Schroeder, alikuwa kansela wa Ujerumani kuanzia 1998 hadi 2005, amekumbwa na shinikizo juu ya kukataa kwake kujiuzulu kutoka majumuku yake makuu ya uongozi katika kampuni za nishati za Urusi za Rosneft na Gazprom.