DFB Pokal: Nani ataibuka mbabe Bayern au Stuttgart ? | Michezo | DW | 01.06.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

DFB Pokal: Nani ataibuka mbabe Bayern au Stuttgart ?

Bayern Munich mabingwa wa Champions League watarajia leo kutimiza ndoto ya kunyakua mataji matatu katika msimu mmoja, wakati watakapopambana na VFB Stuttgart leo(01.06.2013)katika kombe la shirikisho,mjini Berlin.

Bayern Munich's coach Jupp Heynckes (2nd R), team captain Phillip Lahm (R), VfB Stuttgart's coach Bruno Labbadia (2nd L) and team captian Serdar Tasci pose next to the German soccer cup (DFB Pokal) trophy during a news conference in Berlin May 31, 2013. Bayern Munich and VfB Stuttgart play the German soccer cup (DFB Pokal) final match on Saturday at the Olympic Stadium in Berlin. REUTERS/Tobias Schwarz (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER)

Kombe la shirikisho DFB Pokal

Mabingwa wa kombe la vilabu bingwa barani Ulaya Bayern Munich wanalenga katika kukamilisha msimu wa kihistoria leo Jumamosi wakati watakapowania kulinyakua taji la tatu msimu huu, wakati watakapojimwaga uwanjani katika fainali ya kombe la shirikisho, DFB Pokal dhidi ya VFB Stuttgart.

Lakini vigogo hao kutoka jimbo la Bavaria wamesikitishwa na kushindwa kuwapo katika kikosi hicho mlinzi wake wa kati Dante katika fainali hiyo leo(01.06.2013) mjini Berlin.

Bayern wamearifiwa na shirikisho la kandanda nchini Brazil CBF kuwa Dante, pamoja na mchezaji wa kati Luiz Gustavo , ni lazima waripoti katika kikosi hicho cha Selesao kabla ya leo Jumamosi jioni siku ya mwisho ambayo wachezaji wote wanatakiwa katika kikosi hicho cha Brazil kinachojitayarisha kuwa wenyeji wa kombe la mabara , Confederation Cup litakaloanza Juni 15 hadi 30.

TURIN, ITALY - APRIL 10: Karl-Heinz Rummenigge, CEO of Munich speaks during the FC Bayern Muenchen gala dinner at the team squad Principi di Piemonte after winning their UEFA Champions League quarter-final second leg match against Juventus Turin on April 10, 2013 in Turin, Italy. (Photo by Alexander Hassenstein/Bongarts/Getty Images)

Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge

Wachezaji na mwenyekiti wasikitishwa

Wachezaji hao wawili wamesikitika kutoshiriki katika fainali hiyo ya DFB Pokal , na mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameuita msimamo wa shirikisho la soka la Brazil kuwa ni kinyume na ubinadamu, usio wa haki na haukubaliki, licha ya kuwa ni Dante pekee ambaye angeingia uwanjani leo jioni kupambana na Stuttgart.

"Nafikiri , naweza kusema, mbinyo uliowekwa si wa kiutu. Naona pia kuwa ni kinyume cha maadili, na pia naona si wa haki, kwasababu wachezaji hao wawili wamewekwa katika nafasi moja , ambayo kwa kweli siwezi kuikubali."

Hakuna timu ya Ujerumani katika Bundesliga ambayo imewahi kushinda mataji matatu katika msimu mmoja, kombe la Ulaya, ligi ya nyumbani pamoja na kombe la taifa, na Bayern inawania kuwa timu ya kwanza nchini Ujerumani kufanya hivyo. Hata hivyo Bayern itakuwa timu ya saba barani Ulaya kuweka rekodi hiyo.

Timu nyingine ambazo zimewahi kutimiza ndoto hiyo ni pamoja na Celtic ya Scotland mwaka 1967, Ajax Amsterdam mwaka 1972, PSV Eindhoven mwaka 1988, Manchester United mwaka 1999, Barcelona mwaka 2009 na Inter Milan mwaka 2010.

Kocha wa VFB Stuttgart Bruno Labbadia hakutaka kuonesha matumaini makubwa dhidi ya Bayern , lakini amesema kuwa huu ni mchezo muhimu kwa watu wote wa Stuttgart.

VfB Stuttgart's coach Bruno Labbadia addresses a news conference in Berlin May 31, 2013. Bayern Munich and VfB Stuttgart play the German soccer cup (DFB Pokal) final match on Saturday at the Olympic Stadium in Berlin. REUTERS/Tobias Schwarz (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER HEADSHOT)

Kocha wa Stuttgart Bruno Labbadia

"Hali hii sio tu ni muhimu sana kwa klabu ya Stuttgart, kwa mji wa Stuttgart, lakini pia hata kwa sisi tunaoshiriki. Tunataka kujaribu kufurahia hali hii. Tunataka kujaribu kuendelea kuwamo katika hali hii ya shauku na furaha. Na baadaye tutaona kile kinachoweza kutokea."

ARCHIV - Das legendäre Maracana-Stadion in Rio de Janeiro (Archivfoto vom 01.05.2009). Der Countdown zur Fußball-Weltmeisterschaft läuft - auch für Brasilien 2014. Mehrere Städte, darunter auch Rio, sind säumig und haben zum 01. März die FIFA-Frist für den Beginn der Bauarbeiten an den WM-Stadien verstreichen lassen. Es gibt nun eine Galgenfrist bis zum 3. Mai, danach aber kein Pardon mehr. EPA/ANTONIO LACERDA (zu dpa-Korr.: WM-Uhr tickt in Brasilien: 'Gelbe Karte' für Säumige vom 08.03.2009) +++(c) dpa - Bildfunk+++

Uwanja maarufu wa Maracana nchini Brazil

Kasheshe Maracana

Mchezo wa kirafiki kati ya Brazil na Uingereza utakaofanyika kesho Jumapili utafanyika baada ya jaji wa mahakama kutengua uamuzi uliotolewa hapo kabla wa kuzuwia mchezo huo kutokana na sababu za kiusalama.

Serikali ya jimbo la Rio de Janeiro imetoa taarifa kuthibitisha uamuzi huo mpya saa chache baada ya jaji Andriana Costa dos Santos kutoa amri siku ya Alhamis kuwa mchezo huo uliopangwa kufanyika katika uwanja uliofanyiwa ukarabati wa Maracana kuwa hauwezi kufanyika.

Taarifa hiyo ilisema kuwa mchezo kati ya Brazil na Uingereza utafanyika Juni 2 na kuna uhakika wa hali zote za usalama.

Mwandishi : Sekione Kitojo / rtre / afpe / ape

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman