1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Deniz Yücel

Deniz Yücel ni mwandishi habari wa Ujerumani mwenye asili ya Uturuki na pia mchapishaji. Amekuwa mchangiaji wa magazeti kadhaa ya Ujerumani, na hasa magazeti ya Die Tageszeitung na Die Welt.

Serikali ya Uturuki imemtuhumu mara kwa mara Yücel kwa kuifanyia ujasusi kwa niaba ya shirika la ujasusi wa nje la Ujerumani BND, kusaidia makundi yanayodaiwa kuwa ya kigaidi ya FETÖ na PKK. Serikali pia ilidai kuwa Yücel aliyasaidia makundi hayo mawili kuchochea vurugu nchini Uturuki. Katika hotuba mwaka 2017, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alimtagaza Yücel kuwa jasusi na siyo mwandishi habari. Februari 14, 2017 mahakama ya Uturuki ilimtia hatiani Yücel na kumfunga kwa ujasusi.