Demnjanjuk
21 Aprili 2009Matangazo
CINCINATTI.
Wizara ya sheria ya Marekani imeiagiza mahakama ya Cincinatti iondoe kipengere cha sheria kinachozuia kutimuliwa Marekani, kwa John Demnjanjuk anaetuhumiwa kuhusika na maangamizi ya wayahudi alfu 29 wakati wa vita kuu vya pili.
Mtuhumiwa huyo alikuwa mlinzi kwenye kambi ambapo mafashisti waliwafunga na kuwaangamiza wayahudi.
Mtu huyo anatakiwa afikishwe mbele ya mahakama , nchini Ujerumani ili ajibu tuhuma hizo zinazomkabili.
Lakini kuletwa Ujerumani kwa Demnjanjuk kumekuwa kunaahirishwa mara kwa mara na mahakama ya Marekani.