1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

David Luiz aongeza mkataba wa mwaka mmoja Arsenal

24 Juni 2020

Beki wa klabu ya Arsenal ya England David Luiz, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea klabu hiyo ya kaskazini mwa London, Jumatano tarehe (24.06.2020)

https://p.dw.com/p/3eGHS
Brasilianischer Nationalspieler David Luiz
Picha: Miguel Schincariol/AFP/Getty Images

Luiz, ambaye ni raia wa Brazili, mwenye umri wa miaka 33, alijiunga na Arsenal akitokea katika klabu ya Chelsea kwa dau la paundi milioni 8, mnamo Agosti mwaka jana.

"David ni mchezaji muhimu kwetu sisi. Amekwishacheza miongoni mwa mechi zetu katika msimu huu na amekuwa muhimu katika timu,” alisema Edu Said, mkurungenzi wa benchi la ufundi na mchezaji wa zamani.

"Pasi zake, mawasiliano yake na timu ndani na nje ya uwanja yanamsaidia kila mtu.”

Wakati hayo yakichomoza kiungo wa kati Dan Ceballos ambaye alisajiliwa na Arsenal kwa mkopo wa dharura kutoka Real Madrid ya Uhispania, amerefusha muda wake wa kuichezea klabu hiyo ya London hadi mwisho wa msimu uliorefushwa wa mwaka 2019, 2020.

Vile vile Walinzi Pablo Mari na Cedric Soares, ambao walitua Arsenal kwa mkopo wa dharura mnampo mwezi Januari mwaka huu ili kuziba pengo lililoachwa na wachezaji wanaouguza majeraha, wamekubaliana kufanya mkataba wao kuwa wa kudumu wakati kutakapofunguliwa dirisha la uhamisho.