1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Damu zaidi yamwagika nchini Irak.

Abdu Said Mtullya8 Agosti 2010

Watu zaidi ya 40 waangamia nchini Irak kutokana na mfululizo wa mashambulio ya mabomu.

https://p.dw.com/p/Of3j
Mashambulio ya kigaidi yaendelea nchini Irak.Picha: AP

BAGHDAD

Watu wasiopungua 43 wameuawa kutokana na mfululizo wa mashambulio yaliyofatiwa na moto mkubwa katika mji wa Basra kusini mwa Irak.

Mkuu wa usalama wa jimbo hilo la kusini Ali El Maliki amesema washambuliaji waliyalipua mabomu matatu sokoni yoliyosababisha moto mkubwa.Habari zaidi kutoka Irak zinasema kuwa watu wengine wasiopungua saba wameuawa baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka katika mji wa Ramadi uliopo umbali wa kilometa karibu mia moja ,magharibi ya Baghdad mji mkuu wa Irak.

Lakini licha ya mshambulio hayo kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Irak amesema wairaki wapo tayari kuchukua jukumu la kuulinda usalama wa nchi yao Kamanda huyo Ray Odierno amesema jeshi la wazalendo wa Irak lina uwezo wa kuikabili changamoto ya kuulinda usalama wa nchi ingawa nchi hiyo bado inakabiliwa na magogoro wa kuunda serikali mpya

Lakini Jenerali Odierno amesema ni muhimu kwa Irak kuunda serikali mpya baada ya kuchelewa kwa miezi kadhaa kufanya hivyo.