Damu inazidi kumwagika nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 16.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Damu inazidi kumwagika nchini Irak

Washington:

Kwa mujibu wa mkuu wa vikosi vya Marekani katika eneo la mashariki ya kati,matumizi ya nguvu nchini Irak yamefurutu na hayavumiliki.Bado hali ya mambo bado si nzuuri amesema mkuu wa uongozi wa kijeshi wa vikosai vyote vya Marekani-CENTCOM jenerali John Abizaid mbele ya wawakilishi wa baraza la congress mjini Washington.Amezungumzia hata hivyo juu ya kuboreka hali ya mambo tangu mwezi Agosti uliopita.Wakati ule jenerali Abizaidi alizungumzia juu ya matumizi ya nguvu kati ya jamii za madhehebu tofauti,akihoji hali hiyo inaweza kuzusha vita vya wenyewe kwa wenyewe.Mjini Baghdad kwenyewe uongozi wa kijeshi wa Marekani umesema „magaidi tisaa wameuwawa na watuhumiwa wengine tisaa kukamatwa kufuatia opereshini ya jeshi la Marekani kusini mwa mji mkuu wa Irak.Wakatai huo huo wanajeshi watatu zaidi wa Marekani wameuliwa na kuifanya idadi ya Marines waliouliwa katika kipindi cha saa 48 kufikia wanajeshi 10.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com